FRESHI NA MAISHA 1- 4

UHAKIKI WA KITABU: FRESHI NA MAISHA 1-4

I. Rekodi za Kibibliografia

Jina la vitabu vinavyohakikiwa hapa ni Freshi naMaisha, kitabu cha kwanza hadi cha nne na vimetungwana Elieshi Lema. Mchapishaji wa vitabu hivi ni E&DLimited na amevipatia namba zifuatazo katika sekwensiaya vitabu duniani (ISBN): Freshi ya Maisha 1,9987-622-64-x, Freshi na Maisha2, 9987-622-65-8,Freshi na Maisha 3,9987-622-66-6,Freshi na Maisha 4,9987-622-67-4.Vitabu vyote vinne vimechapwa mwaka wa2005.Kitabu cha kwanza kina kurasa 34, Kitabu cha pilikina kurasa 37, Kitabu cha tatu kina kurasa 52 nakitabu cha nne kina kurasa 64.Na anayevihakiki sasahivi ni Padre Privatus Karugendo.

II. Utangulizi

Vitabu hivi vilivyoithinishwa na EMAC tarehe 10 mwezi wa 5 mwaka 2005 kuwa vitabu vya Ziada kwa ajili yaDarasa la Tano na la Saba katika shule za msinginchini Tanzania, vimeandikwa kwa aina yake.Kila kitabukina jina lilelile la Freshi na Maisha,lakini ujumbeni tofauti lakini ulioungana katika mwendelezo.Wahusika ni wale wale. Kitabu cha kwanza kinabebaujumbe wa “Jipende”: “ Maisha anaishi katika familiayenye upendo na amani, ana bidii ya kazi, nyumbani nashuleni. Maisha ameanza kupata dalili za kukua.Changamoto mpya zinamkabili. Anakutana na Freshianayekuwa rafiki yake. Freshi anamfunulia Maishauwanja wa maarifa ya stadi za maisha kuhusukujipenda”.Kitabu cha pili kinabeba ujumbe wa “Jilinde”: “ Freshiameendelea kuwa rafiki mkuu wa Maisha.Katika kitabuhiki Freshi anamwezesha Maisha kuona jinsi mwili wabinadamu ulivyo wa kipekee, na jinsi ambavyo ni wajibuwetu kuulinda dhidi yamagonjwa yote, na hasa UKIMWI.”Kitabu cha tatu kinabeba ujumbe wa “Jijue”: “Mojawapoya stadi kuu za maisha ni kufahamu jinsi ya kutumiaakili yako kunufaisha maisha yako, mahali popoteulipo.Uwe mtendaji,siyo mtedewa, ili ujielewe zaidi,ujiamini zaidi, ufanye mambo makubwa na udhibitimwelekeo wa maisha yako”Kitabu cha nne kinabeba ujumbe wa “Jithamini”: “Maisha amefika Darasa la Saba. Amekua kimwili na akiliimepevuka kiasi. Ameanza kujithamini na kutambuamazingira tofauti yanayomzunguka pamoja na changamotozake. Maisha amegundua kwamba wazazi ni wazito katikakuongea masuala ya ngono na vijana wao. Hali hiiimewaweka vijana njia panda, huku jamii ikiwainajiundia ngao ya ukimya kuhusu masuala nyeti kamahaya”.Vitabu vyote vimegawanywa kwenye sura fupi fupizikifuatwa na maswali ya majadiliano na picha mbalimbali zinazosaidia kufikisha ujumbe. Kitabu cha kwanzakina sura Saba fupi, kitabu cha pili na cha tatu vinasura nane ambazo ni vupi pia na kitabu cha nne kinasura kuminamoja. Katika aya zifuatazo nitatoamuhtasari na tathmini yake, lakini baada ya kudokezamazingira yanayovizunguka vitabu hivi.

III. Mazingira yanayovizunguka vitabu hivi.

UKIMWI ni janga la kitaifa. Taifa letu lina mikakatimbali mbali ya kupambana na ugonjwa huu. Wataalamwanakubaliana kwamba kwa kiasi kikubwa ugonjwa huuunaenea kupitia tendo la ngono. Tendo hili linapendwakwa wingi, lakini kilamtu anapenda alifanye katikauficho. Hakuna aliyetayari kuliongelea kwa uwazi.Wazazi hawataki kuliongea na watoto wao, ingawa kunaushahidi wa kutosha kwamba vijana hadi watoto wadogowa miaka 10 wanatenda tendo hili. Nyakati tulizomo,maadili yameporomoka, ngono kimekuwa kitu cha kawaida.Mbaya zaidi vijana wetu wameachwa kuogelea bilamwongozo wa maisha yao. Wazazi wanaogopa kuongea nakujadiliana na watoto wao juu ya mahusiano, juu yamabadiliko katia miili yao, juu ya kupenda na kupendwana hasa juu ya kujikinga na ugonjwa huu hatari.Kama anavyosema mwandishi: “ Lakini kwa sababu yamabadiliko ya jamii kiuchumi na kisiasa, pamoja namwingiliano wa hali ya juu wa tamaduni na amali zajamii tofauti, mifumo ya jadi yaliyoongoza mahusianokatika jamii yamefifia kabisa. Hivyo, katika mudamwingi, vijana wanajilea wenyewe. Vijiwe vyao vimekuwataasisi. Wanajijengea amali zinazoongoza matendo yaokatika mahusiano ya kila siku. Wanabuni lugha yao yakujieleza katika jamii iliyojaa utenganisho. Katikakujilea huko,vijana wengine wanajiona wajanja kwasababu ya uzoefu uliojengeka katika kufanya majaribio,hata kama ni uzoefu potofu. Wanaokuwa na ushawishimkubwa na wanawarubuni wenzao kirahisi” Freshi yaMaisha 4, uk 31-32.Serikali nayo imeshindwa kuwa na mfumo wa wazi wakufundisha maadili na kuwasaidia vijana kujitambua nakujithamini. Mashirika ya kidini pia yameshindwa.Hatuoni mfumo wao kuhusu malezi ya vijana na swalazima la maadili na kujingina na UKIMWI.Mwandishi wa vitabu vya Freshi na Maisha, aliandikakitabu cha hadithi ya “Parched Earth”. Kitabu hikikina mafundisho juu ya vijana kujitambua, kuwatambuawengine na kwa pamoja kushirikiana kujenga mahusianoyaliyo bora kwa lengo la kulinda uhai na hasakupambana na ugonjwa wa UKIMWI. Baada ya kukisomakitabu hikili, nilimshauri mwandishi atunge vitabu kwalugha ya kiswahili, ili viwe msaada wa kuwafundishawatoto wetu namna ya kujilinda, kujipenda nakujithamini. Jibu la mwandishi ni zawadi ya vitabuvinne, vya Freshi na Maisha, ninavyovifanyia uhakikisiku ya leo. Wakati ninampatia ushauri, kumbe yeyealishaviandika na vinatumika kwenye shule za msingi!Huu ni mchango mkubwa na wa kuingwa.Kabla ya kuviandika vitabu hivi mwandishi alifanyautafiti wa akina. Alifanya majadiliano nakuongeanawatu mbali mbali,pia alichimbua vitabu vingi.Hapakuna baadhi ya vitabu alivyovitumia wakati akiandaaFreshi ya Maisha: Choosing Good Health 5&6,Scott,Forestman& Co.,1983; Soul City: Living Positively withHIV and AIDS; Family Medical Encyclopedia, AnIllustrated Guide, Hamlyn, 1983; Prescription forNutritional Hearing, Avery Publishing Group,1997; AllAbout the Human Body, Random House,1958.Ingawa mwandishi ametumia vitabu mbali mbali wakatiakiaandaa Freshi na Maisha,na kufanya majadiliano nawatu wengi, ubunifu wote ni wake na mapungufu yoteyanayojitokeza kwenye vitabu hivi ni mzigo wakemwenyewe!

IV. Muhtasari wa vitabu

Kitabu cha kwanza; Freshi na Maisha 1, kina ujumbe wa“Jipende”. Kitabu hiki ndicho kinachofungua safari yamaisha ya msichana Maisha, anayeishi katika familiayenye upendo na amani, ana bidii ya kazi nyumbani nashuleni. Binti huyu ameanza kupata dalili za kukua.Changamoto mpya zinamkabili.Maisha, anaanza kutafakari juu ya maisha yake: “Hivikukua maanake nini?”, “ Hivi, watu hukua mwili tu, ausehemu nyingine nazo hubadilika?” (Uk 2).Wakati Maisha, akiwa amezama kwenye tafakuri juu yamaisha yake, anakutana na rafiki yake. Huyu rafikijina lake ni Freshi. Huyu Freshi, anajitokeza kwanamna ya miujiza. Anajitokeza katika umbo la jiwe.Huyu ni rafiki ambaye ni mshauri wa kiroho. Watuwengine wanampatia jina la kipaji fiche ndani mwa kilabinadamu. Kwenye mazingira Fulani, huyu anaweza kuitwamalaika mlinzi au roho mtakatifu. Rafiki huyu nisilika iliyomo ndani mwa kila binadamu yenye nguvu naufahamu isiyohitaji kufundishwa. Huyo ndiye Freshi,rafiki wa maisha, anayemwongoza kujipenda, kujilinda,kujijua na kujithamini.Freshi, anamfunulia Maisha, ukweli wa maarifa kwambakujipenda ni ufunguo wa safari ndefu ya kila kijanakuelekea kujilinda, kujijua na kujithamini. Kwambakujipenda kunaanza na mtu kuangalia usafi wa mwiliwake, usafi wa mazingira yake na kutambua kwamba mwilini muhimu na maalumu, nivyo ni lazima kuulinda dhidiya magonjwa.Maisha, anasikiliza ushauri wa Freshi.Anakuwa msafiyeye mwenyewe, anatunza usafi nyumbani na sehemuanakofanyia biashara mama yake. Shuleni anakuwa mfanowa kuigwa katika usafi.Kitabu kina maswali mengi ya majadiliano. Kila baadaya sura kuna maswali zaidi ya matatu. Mfano wa maswalini kama: Taja mabadiliko matatu ambayo yanaoneshakwamba msichana au mvulana amepevuka. Halafu jadili narafiki yako: je, kupevuka maana yake ni nini?, Mwelezerafiki yako, kujipenda maana yake ni nini? Kwa niniFreshi alimpa Maisha uwezo wa kugeuza takataka nauchafu kuwa kitisho? Taja madhara matatu unayoyajuayanayotokana na mazingira machafu.Kitabu cha pili, Freshi na Maisha 2, kina ujumbe wa“Jilinde”. Freshi, anaendelea kumpatia Maisha,maarifa. Maisha anatambua kwamba mwili wa binadamu niwa kipekee na kwamba ni wajibu wa kila binadamukuulinda mwili dhidi ya magonjwa, na hasa UKIMWI.“Lakini kwa kifupi, mwili wako ni kama mashine. Sehemuzake tofauti hufanya kazi kwa pamoja na kwakutegemeana. Lakini mwili wako ni mashine hai, yenyeakili asili ya kupanga, kuratibu, kutathmini nakujilinda” Freshi na Maisha 2 uk 23.Kitabu kinaelezea kwa lugha nyepesi jinsi mwili wabinadamu unavyofanya kazi: Mfumo wa mifupa na viungo,mfumo wa misuli, mfumo wa mzunguko wa damu na hewa,mfumo wa kusaga chakula, mvumo wa neva, mfumounaoshughulikia ulinzi wa mwili na mfumo wa hisia.Kitabu hiki pia kina maswali ya majadiliano kila baadaya sura.Kitabu cha tatu, Freshi na Maisha 3, kina ujumbe wa“Jijue”. Kitabu hiki kinaelezea kwamba mojawapo yastadi kuu za maisha ni kufahamu jinsi ya kutumia akiliyako kunufaisha maisha yako, mahali popote ulipo.Yaani mtu awe mtendaji, siyo mtendewa ili mtu ajielewezaidi, ajiamini zaidi, afanye mambo makubwa na awe naudhibiti wa mwelekeo wa maisha yake.“ Kujijua kunaanza na nafsi yako. Unajichunguza wewemwemyewe ulivyo, kwa kujiona jinsi unavyoishi nafamilia yako, rafiki zako na watu kwa ujumla. Yaleutakayopata kutoka kwa wengine, yanakuongezea maarifajuu yako, au yanakupa changamoto ya kubadilika, auyanakazia ukweli unaoufahamu tayari” Freshi na Maisha3 uk 29.Katika kitabu hiki, Freshi, anamfunulia Maisha, ukwelikwamba maisha ya binadamu yanaongozwa na Ubongo.Ubongo umechorwa na kuonyesha kila sehemu ya ubongo nakazi zake:“ Kichwani mwako Maisha, kuna kitu kinachoitwa ubongo.Ubongo ni ogani ya miujiza tupu. Wasomi wameutafitisana, lakini mpaka sasa mambo mengi yanayohusu uwezowa ubongo wa binadamu hayajafahamika. Lakini hukondiko kila tendo la mwili wako linakoratibiwa,tanfsiriwa na utekelezaji wake kuamrishwa.” Freshi naMiasha 3 uk 46.Kama ilivyokwa kitabu cha kwanza na chapili, kitabucha tatu pia kina maswali mengi ya majadiliano.Kitabu cha nne, Freshi na Maisha 4, kina ujumbe wa“Jithamini”. Hapa Maisha amefika Darasa la Saba.Amekua kimwili na akili imepefuka kiasi. Ameanzakujithamini na kutambua mazingira tofautiyanayomzunguka pamoja na changamoto zake. Maishaamegundua kwamba wazazi ni wazito katika kuongeamasuala ya ngono na vijana wao. Hali hii imewawekavijana njia panda, huku jamii ikiwa inajiundia ngao yaukimya kuhusu masuala nyeti kama haya.“Vijana wanahitaji stadi za maisha, siyo tu kwakujikinga na UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa.Wanazihitaji stadi hizo kama mhimili wa maendeleo yao.Stadi za maisha zitakazowawezesha kufahamu wanachotakamaishani, jinsi ya kukipata na jinsi ya kukilinda nakukiendeleza baada ya kukipata”Freshi na maisha 4 uk47.“ Alaa, sasa naanza kumpatapata Freshi! kumbekujithamini ni kufanya vitu kibao.Kujithamini nikujifanyia kila jambo zuri: kuwa msafi, kula vizuri,kuweka mazingira safi, kuwa na uelewa wa mambo muhimukwa maendeleo yako, kujijua ili uweze kuwa chachu yamaendeleo yako na jamii yako, hapo ulipo.” Freshi naMaisha 4 uk 48.Kitabu cha nne, nacho kina maswali ya majadiliano.Swali lenye mvuto katika kitabu hiki ni hili: Tajamambo mawili abayo siyo rahisi kuyazungumza na wazaziwako. Jadili mambo hayo na rariki yako, kasha mjaribukubuni mbinu ya kuyazungumza na wazazi.V. Tathmini ya vitabu hiviBaada ya kuona muhtasari huu sasa nifanye tathmini yakazi hii aliyoifanya Mama Elieshi Lema. Niungamekwamba wakati mwingine ni vigumu kufanya tathmini yamawazo ya mtu ambaye kwa kiasi Fulani mnakubaliana kwamambo mengi. Nitajitahidi kuwa mwaminifu kwa kilekilichoandikwa katika vitabu vya Freshi na Maisha!Awali ya yote lazima niseme kwamba, kwa kuangaliahadhira anayoikusudia, vitabu hivi vinasisimua sanakutokana na mtindo alioutumia mwandishi. Ni mtindo wasura fupi fupi, kutumia miujiza ya maisha ya kilasiku, picha na maswali ya majadiliano.Pili, ni wazi kwamba mwandishi amefanikiwa kutimizaLengo Lake, yaani kubainisha na kisha kutoa majibukamilifu kwa changamoto zinazowakabili vijana nawalezi wao katika nyakati hizi tulizomo.Tatu, mwandishi amefanikiwa kutoa mchango mkubwakatika kufundisha maadili kwa vijana wetu. Amevumbuakitu ambacho hakikuwepo. Mfumo wa kufundisha kwakusoma vitabu, kuuliza maswali na kujadiliana.Mwandishi anasisitiza kwamba elimu inapatikana kwanjia ya kusoma vitabu. Msisitizo huu unajitokeza sanakwenye kitabu cha nne cha Jithamini.Nne, mwandishi amefanikiwa kutumia lugha nyepesi namifano hai kuelezea mambo magumu. Ameonyesha mbinuambazo vijana wanaweza kuzitumia kufanya majadilianona wazazi wao. Wale wanaoshindwa kuongea na wazazi waowanaweza kutumia mtindo wa kuandika kwenye daftarimaswali, na wazazi wanajibu kwa kuandika: “kwa wananguRobert na Richard, Hamtaweza kukimbia au kuyachengamaisha. Mazungumzo ya ana kwa ana yamewashinda.Tujaribu maandishi. Awapendaye, Mama”. Freshi naMaisha 4, uk 38.

VI. Hitimisho

Vitabu hivi vinasomwa kwenye shule za msingi. Hivivinaitwa vitabu vya watoto. Inawezekana na mwandishi,aliwaandikia watoto. Lakini ukivisoma kwa makini,unagundua kwamba hivi si vitabu vya watoto, hivi ni vitabu vya watanzania wote na hasa watu wazima!Kwa maoni yangu, vitabu hivi ni muhimu kwa watuwazima. Ni muhimu kila mzazi kuwa na vitabu hivinyumbani kwake, avisome na kuviweka kichwani, baadayeafanye kazi ya kuwasimulia watoto au asome na watotowake na kufanya majadiliano.Ukiangalia mpangilio wa vitabu vyenyewe: Jipende,Jilinde, Jijue, na Jithamini, utaona lengo zima lakutaka familia na jamii nzima ya watanzania kuanzishamazungumzo na majadiliano juu ya maadili. Namazungumzo haya ni lazima yaanzishwe na watu wazimawenye uzoefu. Ni lazima yaanzishwe na akina Freshi.Freshi, rafiki wa Maisha,ni changamotokubwa.Mwandishi, amemchora na kumwingiza katikahadidhi za miujiza.Amefanikiwa vizuri sana na ujumbeunafika. Ukweli unabaki kwamba Freshi, ni rafiki wakila binadamu. Kila mtu ana malaika wake mlinzi, kilamtu ana kipaji fiche ndani mwake. Kazi iliyo mbele yakila mtu ni kukikuza kipaji fiche, ni kukubalikumsikiliza malaika wake mlizi. Tunaona mambo yaMaisha, yanakwenda vizuri baada ya kukubalikumsikiliza rafiki yake Freshi. Fundisho tunalolipatani kwamba kila mtu akikubali kumsikiliza malaika wakemlizi, mambo yanakwenda vizuri. Huu ndio ujumbe mzitotunaoupata kutoka kwenye vitabu hivi vya Freshi naMaisha.Vitabu vya Freshi na Maisha, vina maswali zaidi150.Maswali haya yakijibiwa, vinaweza kuandikwa itabuvingine zaidi ya vinne. Huu unaweza kuwa mchangomkubwa wa kuboresha maadili katika jamii yetu. Kwanjia hii tunaweza kupambana na ugonjwa wa UKIMWI.Mama Elieshi Lema, anatutoa kwenye hatua ya kulalamikana kunyosheana vidole juu ya maadili na kutuingizakwenye hatua ya kutenda. Wakati ni huu, timiza wajibuwako! Nunua vitabu, soma na watoto wako, fanyamajadiliano na kukubali kumsikiliza malaika mlinzi!Pongezi nyingi zimwendee Mama Elieshi Lema,aliyeonyesha ubunifu mkubwa wa kuelezea mambo magumukwa lugha nyepesi. Ni matumaini yetu kwamba mto wahekima bado unatiririka kichwani mwake, hivyotunategemea atuandikie tena Freshi na Maisha 5 hadi10. Kwa mtindo wake wa kuandika vitabu hivi vinawezakuendelea bila ya kikomo!

Na,
Padri Privatus Karugendo.

0 comments:

Post a Comment