NAJITAMBULISHA

Ndugu wasomaji wangu, hatimaye nimeweza kujiunga na mtandao huu wa Blog. Ndugu yangu Ndesanjo Macha, alinikaribisha siku nyingi kujiunga na Blog, lakini nilikuwa ninashindwa kwa vile sikuwa na Internet nyumbani. Kwa vile Mungu ni mwema, nimepata bahati ya kuwa na Internet nyumbani.

Kwa kuanzia, nitahakikisha ninaweka makala zangu za nyuma, kuanzia mwaka wa 2004. Nitakuwa mwaminifu kuziweka kama zilivyo bila kubadilisha kitu.Niliandika makala kuanzia mwaka 1996. Nitajitahidi sana kuzitafuta na zile makala za nyuma na kuziweka kwenye Blog hii. Hivyo wale waliokuwa hawapati makala zangu, watazipata zote.

Nawatakia usomaji mzuri, na pia nategemea kupata maoni ya kujenga.
Nawatakia kazi njema.
Ndugu yenu,
Padri Privatus Karugendo.

3 comments:

JM said...

Hello Privatus,

Its great to see your blog online. I look forward to reading more and following your posts.

best,
Julian

Simon Kitururu said...

Asante kwa kujiunga na BLOGU!

Tuko wengi ambao tulikuwa tunapata shida kidogo kuzipata MAKALA zako zenye SHULE!
Karibu sana ingawa nimechelewa kidogo kustukia uwepo wa Blogu HII!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Karibu sana Pd. Karugendo.

Naungana na Mt. Simon kukukaribisha

Post a Comment