UKOO WA ABAYANGO WA NTOBORA- KARAGWE.

Ukoo wa Abayango wa  Ntobora, ambao leo hii  wanaishi katika vijiji vya: Kashebe, Ntobora, Bweranyange,Kiruruma, Kabindi, Kibondo Nyamitoko, Kibondo Omukashenye, Milanda na Katoro Bukoba wana historia ndefu ambayo wengi wao wanaamini imeanzia Onkole Uganda, na wengine wanafikiri kwamba ni mbali zaidi kama vile Ethiopia na Misri?
Inasemekana kwenye miaka ya 1885, Wayango hawa walitoka Ankole na kuishi Kijiji cha Kibona-Karagwe. Wakiwa Kibona, watoto wawili mapacha walizaliwa. Watoto hawa ni Ruhinda na Kayango. Ruhinda akiwa Kato na Kayango akiwa kakuru. Historia hii haielezi vizuri mapacha hawa walizaliwa na nani. Hivyo bado kuna kazi kubwa ya kihistoria kutafuta ukweli huu. Kuna haja pia kusoma vitabu vingine vya historia ya Karagwe ili kubaini kama hawa Ruhinda na Kayango, wanatajwa kwenye historia ya Karagwe. Pia ni muhimu kufahamu huyu Ruhinda anayetajwa hapa ni Ruhinda yupi na Ruhinda wa ngapi?
Ruhinda na Kayango, walihama kutoka Kibona na kwenda Bweranyange. Ruhinda akawa mtawala (Omukama) na Kayango, ambaye ndiye alikuwa mkubwa akapewa kazi ya kumlinda mdogo wake; na kuelekezwa aende kuishi katika kijiji cha Ntobora. Kutokea huko akawa anaandaa ulinzi wa mfalme Ruhinda.
Kayango, aliyekwenda kuishi Ntobora, ndiye chimbuko la Wayango wa Ntobora. Hivyo wayango waliendelea kuishi Ntobora hadi 1935, wakati wakoloni walipotaka watu wawe karibu na huduma. Waliendesha zoezi la kuwahamisha (Fulula) watu kutoka vijiji vilivyokuwa mbali kama vya Ntobora na kuhamia vijiji vya karibu kama vile Kashebe na Milanda.
Wazee wa ukoo huu wanaokumbukwa, ambao wanachimbuka kwa Kayango ni Mugarula alimzaa Muyango, Muyango akamzaa Ituza, Ituza akamzaa Kwajaba, Kwajaba akamzaa Rujuguru, Rujuguru akamzaa Rwabuhaya, na Rwabuhaya akawaza  Birusya, Kalyao na Rushenshe.
Bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kubaini historia hii. Swali la kujiuliza, hii ni historia ya kweli au ni ngano? Rujuguru, alimzaa mtoto mmoja tu? Je yeye hakuwa na ndugu? Na jina lake lina maana gani? Maana kihistoria majina yalikuwa na maana Fulani katika historia ya ukoo au maisha ya mtu husika. Je Rwabuhaya, ambaye ndiye chimbuko la karibu, jina lake Rwabuhaya, lina uhusiano gani na wahaya? Na je huyu Rwabuhaya alizaliwa peke yake? Hakuwa na ndugu?
Kutoka Kashebe, wayango  walisambaa vijiji vya Kabindi, Kibondo, Milanda na Katoro Bukoba. Watoto wa Rwabuhaya:Birusya , Kalyao nda Rushenshe ndo wameusambaza ukoo huu wa wayango wa Ntobora:

1.     UZAO WA BIRUSYA
Birusya alikuwa na wanawake watatu:
·        Mke wa kwanza wa Birusya aliwazaa:
- Katesigwa
- Byekwaso
- Venant
- Verediana
- Godeliva

A.   Katesigwa naye alioa wanawake wawili:
Mke wa Kwanza wa Katesigwa waliwazaa:
         - Petro
       - Cyrlidion
       - Protase
       - Cypridion
       - Gervas
       - Sefrosa
Mke wa pili wa Katesigwa aliwazaa:
        - Lucia
        - Angelina
        - Paskasia
        - Felista
        - Dr. Rose.
B. Byekwaso naye alioa wanawake wawili:
Mke wa kwanza wa Byekwaso amewazaa:
       - Veronica.
      -   Victoria
       -   Majaliwa
       -   Regina
       -   Rose
       -    Anna
       -    Jasntha
      
Mke wa pili wa Byekwaso amewazaa:
       - Savera
      - Desdery
      - David
      - Dickson
      - Serapia
      - Stella
      - Secunda
C. Venant amewazaa:
   - Padri Stephano Birusya
   - Clodward?
   - Albert
   - Marius
   - Munyasi
   - Onesmo
D. Verediana amewazaa:
    - Mary
    - Josephat
   -  Dr. Longino
   -  Padri Kagengele
   - Padri Nicodemus.
   - Madaraka
   - Johnbosco
E. Godelva amewazaa:
 - Seventine
 -  Clementina
 -  Esther
  - Salvatory
  -  Dr.Respius
  -  Nestory
  -  Annanias
  -  Virginia
 -  Juritha
 -  Dorise.

·        Mke wa pili wa Birusya aliwazaa:
- Rwabutondogoro= Huyu ndiye baba yake na Sr Monica
- Kakwangali
- Katibagana
- Mukabagande
- Kigunila

·        Mke wa tatu wa Birusya aliwazaa:
Tinuga, Mukabatabazi na Warwo?
A. Tinuga akawazaa:
- Cosmas
- Marehemu Sista
- Bibiana
- Jacob
- Marehemu Agnes
- Anselim
- Martha.
B. Mukabatabazi akawazaa...?
C. Warwo akawazaa...(Hawa ni wayango wako Kiruruma)

2.     UZAO WA KALYAO
Kalyao, aliwazaa:
·        Muzahura
·        Kwajaba
·         Kashumi
·        Kilomba
·        Tindyebwa (Alipotea)
·        Mukabatunzi
·        Tibashemelerwa
·        Chibahangaile.

A.   Muzahura akawazaa:
- Kamuhanda
- Rwanjungi
- Kengoro?

B.   Kwajaba akawazaa:
- Lukanyanga Kwajaba
- Kakabile
- Bujune
- Richard
- Alfred
- Tibaitwa (Alipotea)

C.   Kashumi akawazaa:
- Joseph Rwihula
- Ponsian Kashumi
- Dominico
-Katebalirwe
- Mukamutala
- Mukenyina

D.   Kilomba akawazaa:
- Lukanshobeza
- Nyamwihula.


3.     Uzao wa Rushenshe

Rushenshe aliwazaa:
- Vedasto Kahoza (Katoro – Bukoba)
- John Igambi (Alipotelea Kenya)
- Kumutemba
- Katoto


Bado kuna mengi ya kutafuta juu ya Ukoo huu wa Wayango wa Ntobora. Jambo la kuzingatia ni kwamba ukoo una mafiga matatu makubwa. Figa la Birusya , Kalyao na Rushenshe. Na kwa mpangilio ambao upo, ni kwamba Figa la Birusya, wengi wao wako Kibondo , Figa la Kalyao, wengi wao wako Milanda na figa la Rushenshe wako Katoro Bukoba.

Wayango hawa wa Milanda na Kibondo wana Mwenyekiti wao wa ukoo ambaye ni Mzee Richard Kwajaba, ambaye anatokana na figa la Kalyao. Na katibu wao ni Bwana Radislaus Cosmas, anayetokana na figa la Birusya.

Ukoo huu ulikuwa na uongozi imara, wakati wa uhai wa Mzee Katesigwa, aliyekuwa mwenyekiti wa Ukoo. Baada ya kifo cha Mzee Katesigwa, ukoo umeanza kuyumba. Kwa maoni ya mwenyekiti wa ukoo huu Mzee Richard Kwajaba, ni kwamba vijana ndio wanauvuruga ukoo huu.

Jitihada hizi mpya za kutafuta historia ya Wayango, zilizobuniwa na padre Vedasto Kwajaba, ambaye anatokana na figa la Kalyao, unalenga kujenga umoja wa ukoo na kurudisha ushirikiano uliokuwepo siku za nyuma.

Ukoo huu umepanuka sana kwa mafiga yote matatu. Na uzao wa mafiga haya matatu umeanza kusambaa na kuishi maeneo mbali mbali. Wengine wanaishi Dar-es-Salaam, Mwanza, Arusha na sehemu nyingine nje ya Tanzania.

Kwa kuweka habari hizi za Wayango wa Ntobora kwenye mtandao, kutasaidia wayango hawa kutambuana na kutunza umoja wa ukoo na kuzuia wanaukoo kuoana.



0 comments:

Post a Comment