MWANA MAMA VICKY  NTETEMA.

Katika safu yetu ya Mwana Mama, leo tunawaletea Vicky Ntetema, mwandishi wa habari wa kimataifa na mtetezi wa haki za Binadamu. Jina la mama huyu lilivuma sana wakati akitangaza shirika la habari la BBC, kwa wengi alijulikana kama mama mwenye sauti nzuri ya kumtoa nyoka pangoni. Kila mtu mpenda habari alitamani kukutana na mama  huyu ambaye daima alitumia kiswahili fasaha na sauti yenye kumvuta mtu kuendelea kumsikiliza.
Mwana mama huyu ni miongoni mwa waandishi wa habari wachache wa Afrika, ambao wamefanikiwa kufanya mahojiano na vingozi mbali mbali wa nchi na watu wengine wengi maarufu  Afrika na duniani kote. Ni mwandishi ambaye hakusita kumbana mtu anayehojiana naye hadi kufanikisha lengo lake au jibu alilolikusudia. Inawezekana aliwaudhi baadhi ya watu waliohojiano nao, lakini hapana shaka kwamba daima aliwafurahisha wasikilizaji wake.
Mbali na mama huyu kusikika akitanga Sauti  ya idhaa ya Kiswahili BBC, jina lake limetokea kuwa maarufu sana alipojitokeza kutangaza na kufichua unyama waliokuwa wakitendewa walemavu wangozi, maalibino. Utafiti alioufanya juu ya suala hili la mauaji ya Albino, ulifichua uwezo wake wa kufanya uchunguzi, ushupavu wa kuusimamia ukweli, kuuelezea na kuutetea. Mauaji ya Albino ni mradi ulioendeshwa na wauaji, ambao walikuwa tayari kutoa roho ya mtu yeyote Yule ambaye angejiingiza kwenye anga zao. Hawa ni matajiri wenye hela ambao wanaweza kumshukughulikia mtu wakati wowote. Vicky Ntetema, hakuogopa vitisho hivyo, aliendelea na uchunguzi wake hadi kufikia hatua ya kutengeneza vipindi na kuvirusha hewani.
Binafsi, nilipat bahati ya kukutana na mama huyu akiwa anafanya utafiti wake kule Magu Mwanza. Unyenyekevu wake, ulinisukuma kuzoeana naye kwa haraka, na sisi mimi tu niliyezoeana naye, bali watu wengi aliokutana nao, na labda ndo maana aliweza kufanikisha utafikti wake ambao ulikuwa umezungukwa na vitisho vya kila aina.

0 comments:

Post a Comment