UTAKATIFU WA NYERERE 2

MAKALA HII ILITOKA KWENYE GAZETI LA TANZANIA DAIMA JUMAPILI 2005.

UTAKATIFU WA NYERERE 2

Kwenye Tazania Daima Jumapili, iliyopita niliandika juu ya Utakatifu wa Baba wa Taifa marehemu Mwalimu Nyerere. Katika makala hiyo niliongelea pia uwezekano wa watakatifu wengine wa Tanzania, kama Marehemu Kadinali Rugambwa, Marehemu Askofu Mwoleka na walei wengine kama vile Marehemu Mzee Kazigo na wengine wengi. Ingawa mimi nilikuwa sihoji ni kwa nini Nyerere, afikiriwe kwanza kabla ya Rugambwa au Mwoleka, inaelekea kuna watu wengine waliohoji jambo hili. Habari iliyoandikwa na Joseph Sabinus na Pd Ubaldus Kidavuri, kwenye gazeti la Kiongozi la Septemba 17-23,2005, inafunua ukweli wenyewe. Kardinali Pengo, anaelezea ni kwa nini aanze Nyerere na si Rugambwa.

Anachoelezea Mwadhama Kardinali Pengo, ni ukweli. Ingawa watanzania walio wengi hawakuujua ukweli huu. Ni kweli kwamba mtu kuwa mtakatifu si lazima awe padri, askofu, kardinali au sista. Kila Mkristu anaweza kuwa mtakatifu. Hata na wale ambao si Wakristu lakini wanaishi maisha ya kumpendeza Mungu, wanaweza kuwa watakatifu.

“Katika Kanisa, mbele ya Mungu na katika utakatifu; hakuna anayetengwa kwa cheo au madaraka, jinsia, umri au kabila…. Hivyo, uwezekano wa Mlei kuwa mtakatifu ni ule ule ulia sawa kabisa na ule wa Papa, Kardinali, Askofu, Padri au mtawa” ( Kiongozi Septemba 17-23.2005).

Jinsi kanisa la Tanzania, lilivyo hadi leo hii ni kwamba walei wanaonekana kuwa katika daraja la tatu. Daraja la kwanza likiwa la Maaskofu, daraja la pili la mapadri, masista na watu wote wenye “daraja takatifu” katika kanisa. Daraja la tatu na la mwisho ni la walei. Na daima kila wakati tunawategemea wale wa daraja la kwanza na la pili kuishi maisha ya utakatifu zaidi. Maisha ya Askofu, Padri au Sista, yanaangaliwa kwa uangalifu zaidi ya mlei aliye katika maisha ndoa. Padri, akijikwaa, inakuwa kelele – lakini mlei akijikwaa na kuwa na vibustiani zaidi ya vitatu, kelele zinakuwa ndogo, au wakati mwingine hakuna kelele kabisa!

Katika hali kama hili, na katika nchi ambayo haijapata mtakatifu hata mmoja, ni lazima watu washangae sana mlei kumtangulia Kardinali wa kwanza Mwafrika, kuwa mtakatifu.

Hakuna utamaduni wa kumtanguliza mlei katika kanisa la Tanzania. Anayebisha, aseme, ili nitoe mifano. Mtu aliyejaribu kuwatanguliza walei katika kanisa la Tanzania, ni marehemu Askofu Christopher Mwoleka. Alipingwa vikali na juhudi zake sasa zimefunikwa na mwili wake kaburini!

Hivyo kwa nchi kama Tanzania, kumtanguliza mlei kunashangaza sana. Si utamaduni, ni jambo jipya! – si baya, lakini lifanyiwe maandalizi. Watu wafundishwe na kuelimishwa zaidi. Wale Wakristu wa daraja la kwanza na la pili nao wafundishwe na kulikubali.

Ukweli mwingine, aliouelezea Mwadhama ni kwamba wakati wa mchakato wa kumtangaza mtu mtakatifu ni lazima watu wajitokeze kusema wazi juu ya maisha ya huyo marehemu, wataje uzuri wake na ubaya wake. Huu ni ukweli ambao watanzania wengi hawakuujua. Ndo tunamtafuta mtakatifu wa kwanza. Jambo hili ni jipya kabisa. Linahitaji mafundisho na teolojia ya pekee. Haiwezekani watu wakalielewa jambo hili kwa habari iliyoandikwa kwenye gazeti la Kiongozi!

“Hili ni jambo la msingi sana… mchakato unapoanza, ni kumuanika mtu.. Hii ni nafasi ya watu kusema uzuri na ubaya wowote katika maisha yake…. Nasisitiza kuwa hakuna atakayelaumiwa au kuchukiwa na Kanisa au kiongozi yeyote wa Kanisa kama atatoa kitu ambacho ni pingamizi. Kama pingamizi zikidhihirika, basi tunanyamaza. Hili sio suala la kificho wala upendeleo wowote. Hatumzibi mtu mdomo; hiki ni kitu cha wazi maana mbele ya Mungu hakuna upendeleo”. (Kiongozi September 17-23,2005).

Ni lazima kubadilisha malezi, ili watu watambue kwamba wanaweza kusema ubaya na uzuri wa viongozi wao wa kiroho. Maana sifa nyingine ya mtakatifu ni kule kufahamu mapungufu yake akiwa hai akayakubali. Ni vigumu mtu kujua mapungufu yake bila kuambiwa na ndugu zake au watu wanaomzunguka. Katika kanisa katoliki la Tanzania, utamaduni huu haupo! Itakuwa vigumu kama mtu ambaye hakuzoezwa kusema baya lolote juu ya kiongozi wake wa kiroho, hata kiongozi wa nchi( Kanisa linakuwa makini sana kuwasema viongozi wa nchi, hata pale ambao ni wazi wamekosea!) aje kulisema baada ya kifo chake.

Ni mambo mengi ambayo ni lazima yafanyike ili watu watambue kwamba wanaweza kusema wazi mambo yanayohusiana na dini yao. Kanisa lenye we lijenge utamaduni wa kukubali makosa na kukosolewa. Ni vigumu kutoa au kushauri watu kufuta kitu ambacho wewe huna wala hufuati.

Mfano tukiangalia vyombo vya habari vya kanisa, daima vinasema mazuri tu ya kanisa. Havigusii mambo mabaya ya kanisa. Kuna mambo mabaya sana ndani ya kanisa ambayo ni lazima yasahihishwe. Si lazima kuyataja lakini mtu aliye makini hata na yule asiyekuwa makini anayajua. Gazeti la Kiongozi, daima linaandika mambo mazuri tu, mambo ya kusifu, yale tu yaliyo chanya Mtu akiandika makala ya kulisahihisha kanisa haichapwi. Ushahidi ni mwingi. Redio Tumaini, inatangaza mazuri, zikitumwa habari za kulisahihisha kanisa hazitolewi. Katika utamaduni kama huu, huwezi kutegemea watu kujitokeza kusema chanya na hasi juu ya Askofu au kiongozi wa kidini.

Hoja nyingine ni kwamba chanya na hasi za mtu, ni za muhimu sana akiwa bado anaishi hapa duniani. Ni bora kumuanika mtu akiwa ana nafasi ya kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya kanisa na taifa. Mchango wake, ndio unarutubisha utakatifu wake.

Nina imani watu wengi wanakubali kwamba mwalimu Nyerere, anastahili kuwa Mtakatifu. Hakuna ubishi. Lakini pia sababu za kumchelewesha Kardinali Rugambwa si za msingi. Ni lazima kuna kitu ndani yake.

Hata tukiachia mbali mambo ya utakatifu. Tuliambiwa kwa Mwadhama Rugambwa, alizikwa kwa muda kwenye kanisa la Kashozi, na kwamba atahamishiwa kwenye kanisa la Bukoba Mjini ifikapo Mwaka 2000, sasa ni 2005, bado mwili wa Mwadhama Rugambwa, haujahamishwa. Kwa maneno mengine bado hajazikwa! Bado hajapata heshima yake ya mwisho. Tatizo ni kwamba Kanisa la Bukoba Mjini, bado linafanyiwa ukarabati. Ukarabati ambao sasa ni zaidi ya miaka 10! Inawezekana Jimbo katoliki la Bukoba, limeshindwa kupata pesa za kumalizia ukarabati. Lakini Mwadhama Rugambwa, alikuwa kipenzi cha watanzania, aliwafanyia mengi. Inawezekana viongozi wa Juu wa Kanisa hawayaoni, lakini watu wa kawaida na hasa walei wanayaona na yanawagusa. Pia makanisa mengi ya Afrika, yalimpenda Mwadhama Rugambwa, Wakristu na watu wengine wa nchi za nje walimpenda Rugambwa. Ukiitishwa mchango wa kulimalizia Kanisa la Bukoba, ili Rugambwa, apumzike kwa amani, ni imani yangu watu wengi watajitokeza kuchangia. Mbona sasa hivi watanzania wanachangia mambo mbali mbali? Walichangia Serengeti Boys, wanachangia kwa wingi matibabu na uchunguzi wa matiti ya akina mama nk.

Hata hivyo hatujawa na watakatifu wengi kiasi cha kusema huyu atangulie na mwingine asubiri. Ni bora Mwadhama Pengo aseme ukweli, kwamba kanisa lilikuwa limepitiwa. Maana hata ukiachia mbali Mwadhama Rugambwa, kuna watu walioishi kitakatifu lakini hakuna jambo ambalo limefanyika hadi leo hii.

Askofu Kilaini, ameandika juu ya watu wengi waliofanya mambo mazuri katika kanisa kwenye kitabu chake (tasnifu) wakati wa digrii yake ya uzamifu. Mbona hakuna lolote liliofanywa juu ya watu hawa? Alipoandika kitabu chake alikuwa padri. Lakini baada ya hapo amekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu katoliki la Tanzania, nafasi ambayo ingemwezesha kufanya mengi juu ya jambo hili, sasa hivi yeye ni Askofu, nafasi inayomwongezea uwezo mwingi zaidi wa kufanya mengi juu ya hili. Swala si kwamba watu wanalalamika kutangulia Nyerere, kabla ya Rugambwa, hoja ni kwamba
Kanisa katoliki la Tanzania kusinzia kwa mambo mengi.

Na,
Padri Privatus Karugendo.

2 comments:

cherry said...

Ndio nimeona makala hii ingawa inaonekana ni ya siku nyingi. Suala la mchakato wa kumtangaza mtu kuwa mtakatifu ni nyeti sana na kuna mambo mengi hayako wazi. Wengine wanachukua miaka mingi kabla ya hata kuanza mchakato lakini mwisho wa siku mchakato unakamilika. Muda hauondoi utakatifu la muhimu ni kuanza mchakato. Kwa mtu wa kawaida kama mimi niliyemfahamu Kardinali Rugambwa tangu nikiwa mdogo nilitegemea pia kuwa mchakato ungekuwa umeanza na unaendelea. Nchi jirani ya Kenya, sitashangaa Marehemu Kardinali Otunga kutangazwa Mtakatifu kabla ya Rugambwa kutokana na umakini unaoendana na mchakato wake. Kanisa Katoliki Tanzania lingekuwa pro-active kuanzisha na au kufuatilia michakato ya watu wanaotajwa kuwa wanaweza kutangazwa watakatifu - marehemu sista Mbawala akiwa mmoja wapo.

Post a Comment