KISIKI KIKAVU

UCHAMBUZI HUU ULICHAPWA KWENYE GAZETI LA TANZANIA DAIMA 2007

UHAKIKI WA KITABU: KISIKI KIKAVU

1. REKODI ZA KIBIBLIOGRAFIA
Jina la kitabu kinachohakikiwa hapa ni Kisiki Kikavuna kimetungwa na Aldin Mutembei. Mchapishaji wakitabu hiki ni E&D Limited na amekipa namba ifuatayokatika sekwensia ya vitabu duniani (ISBN) 9987 411347. Kimechapishwa mwaka 2005 kikiwa na kurasa 72. Naanayekihakiki sasa hivi katika safu hii ya Kisima chaUjuzi ni mimi Padri Privatus Karugendo.

II. UTANGULIZI.

Hii ni hadithi ya kubuni na mhusika mkubwa akiwaKalabweli. Mazingira ya hadidhi hii ni Mkoa wa Kagera,Nchi ya Uganda (vita na mpakani) na Dar-es-salaam.Hadithi inafunua historia ya Ugonjwa wa Ukimwi, mkoaniKagera.Kalabweli alitarajia kuwa angewatunza wazazi wake,dada na wadogo zake. Na kweli Kalabweli alifanikiwakatika biashara, akashamiri, akapenda na kupendwa,akaijua pesa.. Kisiki Kikavu kinatufunulia maisha yaKalabweli ambayo yamebeba historia ya UKIMWI hukomkoani Kagera. Historia iliyoanzia katika umasikiniuliofuatia vita vya Iddi Amin, hali iliyozaa biasharaya magendo na maisha ya starehe iliyokithiri. UKIMWIukabisha hodi ukapatiwa majina; Juliana, Silimu, Ninjank.Kwa maneno ya Profesa F.E.M.K Senkoro, Mwanafasihi waIdara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam,Kisiki Kikavu kinaweka wazi udhaifu wetu katikakukabili changamoto za maisha. Jinsi mtu anavyozidikusoma Kisiki Kikavu ndivyo anavyoona kwambahistoria, siasa, mila na uchumi vimeshikamana katikakuibua na kutandawaza janga la UKIMWI, na hapo ndipomtu anapogundua Ukavu wa fikra za mwadamu. Na kwamba hii ni riwaya ya aina yake inayochambua taadhira yaVVU, uelewa wa watu, ukubalifu wao na jinsi tabiazinavyobadilika kwa wakati, mahali na kwa rika.Kitabu kina sura nane na zimepewa majina badala yanamba. Majina haya ni: Handaki, Kikomela, Ihembe,Juliana, Silimu, Ninja, Kadi Nyekundu na KisikiKikavu. Majina yote kwa namna moja ama nyingineyanahusiana na Ugonjwa wa UKIMWI. Ni historia yaugonjwa huu ulivyoendelea kujifunua miongoni mwa jamiiya watu wa mkoa wa Kagera na baadaye kuenea hadiDar-es-salaam. Katika aya zifuatazo nitatoa muhtasarina tathmini ya kitabu.

III. MUTASARI WA KITABU.
Sura ya Kwanza, inayobeba jina la Handaki, linaelezeamaisha ya watu wa Kagera, mara baada ya vita yaKagera. Vita iliacha nyuma Mahandaki, ambayo watuwalikuwa wakiyatumia kujificha maadui na ndege za IddiAmin, zilizokuwa zikitupa mabomu. Baada ya vitamahandaki, yakawa maficho ya nyoka na chatu. Familiaya Mzee Kakwezi, inaanza kuonja machungu ya mahandaki.Mtoto Keisho, anamezwa na chatu ndani ya handaki.Katika sura hii msomaji anaonja falsafa ya mwandishi.Maana mahandaki yanakuwa na maana pana zaidi yamashimo yaliyochimbwa kwa nia ya kujificha maadui.Katika sura hii, mwandishi anatuaandaa ili tuonematokeo ya vita. Maana si mahaandaki tu, baada ya vitamaisha yalikuwa magumu, serikali ilitangaza miezi 18,ya kufunga mikanda. Hali hii ilipelekea chanzo chabiashara ya magendo iliyokuwa ikifanyika kati yaUganda na Tanzania. Biashara hii, ilileta neema namaafa.Sura ya pili, inayobeba jina la Kikomela, inatufunuliahali ya biashara ya magendo ilivyofanyika. Kikomela,ni soko lililokuwa likiendesha biashara ya magendompakani mwa Uganda na Tanzania. " Barabarani, na hasa kwenye njia panda, vile vizuizivilivyowekwa wakati wa vita kuwashika wapelelezi namaadui wengine, sasa vikageuzwa vizuizi vya kuwashikawafanya magendo. Vizuizi hivyo vilileta kero kubwa kwaraia wasio na hatia" (uk 11). Vijana waliacha shule na kuanza kufanya biashara yamagendo. Kwa maelezo ya mwandishi, magendo ililetaneema na kuwafanya watu kusahau hali ngumu ya vita.Pesa za magendo ziliwafanya vijana kuponda raha,kunywa na kugeukia uzinzi.Sura ya tatu, inayobeba jina la Ihembe, inatufunuliawagonjwa wa kwanza kupata ugonjwa wa UKIMWI. Kwa vilewagonjwa mwanzoni ni wale waliokuwa wakienda kufanyabiashara kule Uganda, iliaminika kwamba walifanyamambo mabaya kule Uganda, na ndiyo maana walipata"Ihembe" (Aina Fulani ya uchawi: " Ndugu zangu zikilizeni. Hapa tumeingiliwa. Hakunamtu ambaye hajui misiba inayotupata siku hizi. Watuwanakufa, wanakufa mmojammoja. Miili yao haisikii dawatena. Huu si ugonjwa. Na hospitalini wameshindwa.Hospitali zote, hata kule Bukoba, wagonjwa wanakwendawanarudishwa. Baada ya muda kifo 'kifo cha ajabu'.Watu hawa kama nilivyoona, wamewadhulumu wenzao hukokwenye biashara zao. Dhuluma ndiyo imeleta vifo hiviHiki ni Kisasi. Ni lazima tufanye kafara. Twendetukamwage kahawa katika mto Kagera." (uk 31).Sura ya nne, Ukimwi unapata jina la Kwanza. Jina hilini Juliana. Hii ilitokana na vitambaa vya nguovilivyojulikana kama Juliana, vilivyokuwa vikitokeaUganda. Vijana waliokuwa wakifanya magendo, waliviuzana kuvivaa vitambaa hivi. Hivyo ugonjwa huu, ambaohaukujulikana ukapata jina la Juliana. Hapa watu wengiwalianza kuambukizwa na kupoteza maisha kwa ugonjwahuuu wa Juliana.Katika sura ya tano mwandishi, anatupatia jina pili laugojwa huu, ambalo lilitokana na namna wagonjwawalivyokuwa wakipungua kabisa na kubaki mifupa.Ugonjwa ukabatizwa Silimu. Na katika sura inayofuata,baada ya ugonjwa huu kusambaa na kuvuka mipaka ya mkoawa Kagera, ukawa na majina mengine kama vile Ninja.Sura ya saba na ya nane zinazobeba majina ya KadiNyekundu na Kisiki Kikavu, zinaonyesha jinsi ugonjwawa IKIMWI, ulivyoenea na kuzagaa na kuacha visikivikavu. Familia ya mzee Kakwezi, iliyoanza kuonjamachungu ya maandaki, inampoteza shujaa wa familiaKalabweli, aliyefanya biashara ya magendo, akapatapesa, akaponda raha hadi akahamia Dar-es-salaam, nakuendelea kuponda raha hadi akafa na huku akiachaidadi ya watu wengi wakimfuata nyuma yake.

IV. THAMINI YA KITABU.

Baada ya kuona muhtasari huu sasa tufanye tathmini yakazi hii aliyoifanya Aldin Mutembei. Awali ya yotelazima niseme kwamba kwa kuangalia hadhiraanayoikusudia, kitabu hiki au niseme hadithi hiiambayo ni ya kubuni inasisimua sana. Mwandishi,amefanikiwa kuchora historia ya ugonjwa wa Ukimwimkoani Kagera na jinsi ulivyosambaa nchi nzima.Inajulikana wazi kwamba mgonjwa wa kwanza hapaTanzania, aligunduliwa mkoani Kagera.Pili, mwandishi amefanikiwa kuonyesha jinsi vita vyaIddi Amini, vilivyoleta maafa mengi. Ugumu wa maishauliofuata baada ya vita, ulisababisha biashara yaMagendo na mwingiliano wa watanzania na waganda ukawamkubwa. Inaaminika kwamba hiyo ndo ilikuwa njia yakuingiza UKIMWI, hapa Tanzania. Labda, nani anajua,bila vita, ugonjwa huu, ungeinga kwa namna nyingine,au ungetukuta tumejiandaa na kuwa na elimu juu yake.Tatu, mwandishi ameonyesha wazi kwamba bila elimu,watu wanaweza kuangamia bila kujua. Mfano unajionyeshakwenye majina ya Ukimwi, mwanzoni walifikirini uchawi,baadaye ikawa Juliana, Sililmu na Ninja. Viongozi wadini walifikiri ni shetani na adhabu kutoka kwa Mungu.Mwandishi, ameyachora haya vizuri kabisa kiasi cha mtuanaposoma, anajional yuko mbele ya mchungaji akipatamahubiri juu ya shetani anayepitia kwenye ugonjwa waUKIMWI. Hapa tunapata fundisho kwamba elimu na utafitini vitu vya msingi.Nne, mwandishi amefanikiwa kuonyesha kwamba historia,siasa, mila na uchumi vimeshikamana katika kuibua nakutandawaza janga la UKIMWI.Tano, mwandishi amefanikiwa kugusa nyanja mbali mbalikatika jamii yetu, amegusia vyuo vyetu na maadiliyanavyochechemea, amegusia familia, serikali, dini nakuonyesha jinsi kila mtu anavyoguswa na ugonjwa huu waUKIMWI.Ingawa hadithi hii ya Bwana Mutembei, inasisimua nakumfanya mtu atafakari mengi na kuwa mwangalifu juu yaugonjwa huu wa hatari, hadithi yake inaisha bila yamatumaini. Kisiki kikavu, hakina maisha na si daliliza matumaini. Wakati huu, si wakati wa kuongeleaKisiki Kikavu, bali shina linalochipuka!Kwa namna ya kushangaza kidogo, Bwana Mutembei,ameamua kutogusia kampeni ya Tosheka naye, acha autumia kinga. Ni kweli mambo haya, hayapunguzi utamu wakitabu. Bado ni kitabu kizuri kukisoma. Ila hadidhiyake ingenoga zaidi kama angejitahidi kuingiza mambokama haya. Kwa vile anaelezea historia ya ugonjwa huu,isingekuwa mbaya kuonyesha na hatua nyinginezilizofikiwa hivi sasa. Hata hivyo hadithi yake ni yahivi karibuni 2005.Matumaini mengine, ambayo yako sasa hivi ni dawa zakurefusha maisha, dawa za kuzuia maambukizo kutoka kwamama kwenda kwa mtoto, na kuna ukweli kwamba siku hizimaambukizi yanapungua baada ya watu kuanza kuufahamuugonjwa huu, na kuacha kufikiri kwamba ni uchawi.Kisiki Kikavu, sasa hivi ni shina linalochipuka!

V. HITISMISHO.

Kwa kuhitimisha, ninawaomba watanzania wakisome kitabucha Kisiki Kikavu, ili wapate mengi kuhusiana naUgonjwa huu wa UKIMWI. Ingawa, hii ni hadithi yakubuni, lakini imesheheni mifano hai ya kutusaidiakupambana na ugonjwa huu wa hatari.Pia ningependa kumshauri Bwana Mutembei, kuandikahadithi nyingine ya Shina linalochipuka. Yeye kamamtafiki wa ugonjwa huu katika mkoa wa Kagera, kwamiaka mingi sasa, anajua ukweli wote kwamba kunamatumaini makubwa. Baada ya giza la Ihembe, Juliana naSilimu kupotea, sasa hivi kuna mwanga mpya namatumaini.

Na,Padri Privatus Karugendo. ____________________________________________________________________________________Don't

0 comments:

Post a Comment